DAY CARE BORA
NDANI YA MOSHI

KARIBU LITTLE SPROUTS 

Tunatoa huduma za kulea watoto na kuandaa matukio ya kufurahisha watoto

KWANINI UTUCHAGUE SISI

Kwanini sisi tunapaswa kuwa day care yako pendwa zaidi ndani ya Moshi

Mazingira salama na yenye ulinzi

Hapa Little Sprouts Moshi tumeweka kipaumbele kwenye ulinzi na usalama wa mtoto wako. Tumechukua tahadhari zote za msingi kuhakikisha ulinzi na usalama wa watoto wako, hii ikiwa ni pamoja na kuwa na kamera za ufuatiliaji wa kinachoendelea hapa kituoni kwetu.

Walimu na wahudumu bora

Timu yetu ina watu wenye uzoefu mkubwa, walipitia mafunzo sahihi na wenye kupenda kutoa huduma bora kwa mtoto wako. Tunaelewa kuwa kila mtoto ana upekee wake na tunafanya bidi kujenga mazingira ya kujifunza.

Program zenye manufaa makubwa

Tunawapa watoto shughuli za kusisimua, mafundisho yanayoendana na umri wao, na kuwajengea kupenda kuwa wachunguzi na wagunduzi. Mtoto wako atajengewa ujuzi muhimu na kuwa na msingi imara wa maisha siku zijazo.

babynew

Milo kamili na Lishe bora

Tunafanya kazi pamoja na wazazi kuunda menyu ambayo imejaa virutubisho muhimu na inayokidhi mahitaji ya lishe ya watoto wanaokua. Kwa kutoa milo bora, tunalenga kuwajengea watoto mazoea ya kula vizuri.

Day care center in Moshi

JINSI YA KUMUANDIKISHA

MTOTO WAKO HAPA LITTLE SPROUTS MOSHI

Hatua ya kwanza ya kumsajili mtoto wako kwenye day care bora ndani ya Moshi - Little Sprouts Moshi ni kupakua na kujaza fomu ya kujiunga. Kisha ututumie kupitia WhatsApp au Barua pepe:

+255767080236 | info@littlesproutsmoshi.com

HUDUMA YETU YA KUKAA NA WATOTO

Sisi sio tuu kwamba ni day care bora ndani ya Moshi, lakini pia ni chaguo la wengi kama kituo cha malezi ya watoto wao.
Tunapokea watoto wadogo kuanzia miezi mitatu. Uwe mwanafunzi, mfanyakazi, au tuu msafiri unayetembelea mji wa Moshi, mlete mtoto wako kwetu na kwa furaha tutakuangalizia mtoto kwa malezi bora iwe kuanzia asubuhi mpaka jioni au iwe tuu kwa masaa machache.

Tupo dakika chache kutoka katikati ya mji hivyo itakua rahisi kwako kumuacha na kumchukua mtoto wako.

The best day care center in Moshi

SHUHUDA

Asanteni jamani kwa kuwa na ratiba nzuri kiukweli mnajitahidi sana. Mungu awabariki sana.
Hongereni sana sana.Mungu awabariki muendelee kuwafundisha maadili tunashukuru mno.Be blessed
Tunashukuru sana kwa kukaa na watoto wetu kwa upendo. Mungu awabariki sana.
Jamani Mungu awabariki sana kwa kazi yenu njema na kwa Kukaa na watoto wetu kwa upendo.
Jamani Mungu awabariki sana kwa kazi nzuri mwanangu sasa hivi anaamka mwenyewe anataka kwenda shule.
Jamani walimu wako vizuri na pia ni wabunifu naona watoto wanamichezo mingi na wanaenjoy sana.God bless you

GALLERY YETU

Picha za shughuli mbalimbali katika day care yetu mjini Moshi

MASWALI YAULIZWAYO MARA KWA MARA

Tunaelewa kama wazazi, mnaweza kuwa na maswali ya muhimu kuhusu huduma zetu. Ili kusaidia kupata taarifa unazohitaji, tumeandaa orodha ya maswali ambayo huulizwa mara kwa mara , na kukupatia majibu mafupi ya kueleweka. Kama hauoni jibu la kile unachotafuta, tafadhali, usisite kuwasiliana nasi moja kwa moja.

Je, una swali?

Tuachie maswali yako na tutakujibu haraka iwezekanavyo.

Little Sprouts Moshi inawakaribisha watoto wenye umri wa miezi 3 hadi miaka 5.

Kituo chetu hufanya kazi kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa kumi na moja na nusu jioni, siku za Jumatatu hadi Ijumaa. Lakini waweza wasiliana na uongozi wa kituo endapo unahitaji huduma zetu nje ya muda huu.

Little Sprouts Moshi tumeweka taratibu makini za kiusalama ikiwa ni pamoja na eneo lenye ulinzi, kamera zenye kufuatilia kinachoendelea kituoni, wafanyakazi wetu wamepitia mafunzo ya kuwajibika katika hali za dharula.

Tunafuata mtaala wenye kujitosheleza ambao umejikita katika kukuza ubunifu, kufikiri kwa makini, stadi za kijamii, na uelewa tamaduni zetu , kupitia shughuli zinazolingana na umri pamoja na kufundisha kupitia michezo.

 

 

Little Sprouts Moshi huwa ipo wazi kipindi mwaka mzima isipokua nyakazi za sikukuu kubwa kubwa. Tutaoa taarifa kwa wazazi endapo itahitajika kufunga wakati wa sikukuu fulani.

Tuna sera ya mawasiliano ya wazi na inayoeleweka. Tumewapa wazazi njia za kuwasiliana nasi kila siku. Njia hizo ni kama vile: mazungumzo ya ana kwa ana na wazazi wanapokuja kuwachukua watoto wao, pia kupitia ujumbe kwa WhatsApp na simu za kawaida. 

Tuna mapenzi makubwa kwa malezi ya watoto, hali inayotusaidia kujitoa na kujituma katika kuhakikisha usalama na ustawi wao. Tumeweka kamera za CCTV katika eneo letu kusaidia kuhakikisha usalama wa watoto. 

Mawasiliano

SAA ZA KAZI

Jumatatu – Ijumaa : Saa 1 asbh – 11:30 jioni. Jumamosi na Jumapili tunafunga

MAHALI TULIPO

Mtaa wa Ushirika, Barabara ya Nkomo, Moshi Mjini, Kilimanjaro

SIMU & WHATSAPP

+255 767 080 236

BARUA PEPE

info@littlesproutsmoshi.com

TUACHIE UJUMBE

Little Sprouts

Kituo chako cha kutunza watoto cha kuaminika ndani ya Moshi na tumejikita kutoa huduma bora ya uangalizi watoto, tukiwapa mazingira salama, yenye kuvutia na kuelimisha. Walezi wetu wenye uzoefu, shughuli zenye kufurahisha watoto, na kujitoa kwetu kweli kweli kuhakikisha ukuaji wa watoto vinatufanya kuwa chaguo bora kwa wazazi wanaotafuta huduma bora kwa watoto wao.

Kampuni

Kuhusu sisi
wasiliana nasi
Mahali tulipo

Huduma

Day Care
Kuangalia watoto
Matukio na shughuli
Jitolee

Blog

Coming soon