KUHUSU SISI

Mwanzo |    Kuhusu sisi

Sisi ni akina nani

Sisi ni kituo kitoacho huduma ya day care na uangalizi wa watoto wa kiwango cha juu, tukiwa na dhamira ya kutoa mazingira yenye upendo na kuvutia ndani ya Moshi. Tukiwa na kipaumbele cha upendo, malezi, na elimu ya utotoni, tunajitahidi kuwafanya watoto wako wajisikie wapo nyumbani.
Little Sprouts Moshi, tunaelewa mahitaji ya kipekee ya kila mtoto na tumepanga programu zetu ili kusaidia ukuaji na maendeleo ya mtoto mmoja mmoja. Timu yetu ya walezi wenye uzoefu na kujitoa haswa, imejawa na mapenzi makubwa ya kujenga mazingira salama na thabiti ambapo watoto wanaweza kuwa wadadisi, kujifunza, na kukua.
Tunathamini mawasiliano ya wazi na wazazi na kuwachukulia kama sehemu muhimu ya safari ya mtoto wao. Timu yetu iko tayari daima kujadili maendeleo ya mtoto wako, kushughulikia wasiwasi wowote, na kushirikiana nawe ili kutoa huduma bora zaidi.

 

UPENDO, MALEZI, USALAMA

Tumejitoa kukuza ukuaji wa jumla wa watoto, tukienzi na kufurahia utofauti wa kila mtoto, na kuwawezesha watoto kuwa watu wenye ujasiri, wenye huruma, na wenye uwezo ambao unafuata maadili na misingi ya maisha ya kiafrika.

SHUHUDA

Asanteni jamani kwa kuwa na ratiba nzuri kiukweli mnajitahidi sana. Mungu awabariki sana.
Hongereni sana sana.Mungu awabariki muendelee kuwafundisha maadili tunashukuru mno.Be blessed
Tunashukuru sana kwa kukaa na watoto wetu kwa upendo. Mungu awabariki sana.
Jamani Mungu awabariki sana kwa kazi yenu njema na kwa Kukaa na watoto wetu kwa upendo.
Jamani Mungu awabariki sana kwa kazi nzuri mwanangu sasa hivi anaamka mwenyewe anataka kwenda shule.
Jamani walimu wako vizuri na pia ni wabunifu naona watoto wanamichezo mingi na wanaenjoy sana.God bless you

Una swali kuhusu sisi?

Little Sprouts

Kituo chako cha kutunza watoto cha kuaminika ndani ya Moshi na tumejikita kutoa huduma bora ya uangalizi watoto, tukiwapa mazingira salama, yenye kuvutia na kuelimisha. Walezi wetu wenye uzoefu, shughuli zenye kufurahisha watoto, na kujitoa kwetu kweli kweli kuhakikisha ukuaji wa watoto vinatufanya kuwa chaguo bora kwa wazazi wanaotafuta huduma bora kwa watoto wao.

Kampuni

Kuhusu sisi
wasiliana nasi
Mahali tulipo

Huduma

Day Care
Kuangalia watoto
Matukio na shughuli
Jitolee

Blog

Coming soon