HUDUMA

Mwanzo |    Huduma zitolewazo

HUDUMA YA DAY CARE

Tunatoa huduma bora za uangalizi wa watoto, elimu, na mazingira yenye kuendana na watoto kujifunza na ukuaji wao.
Kituo chetu kina vifaa vya kisasa na kimepangiliwa kukuza udadisi, ubunifu, na kuwajenga waweze kuwa wenye kushirikiana katika jamii. Mtaala wetu unazingatia elimu ya utotoni, ukihusisha masomo kama lugha, hesabu, sayansi, sanaa, na muziki. Usalama ni jambo la kipaumbele, na kuna udhibiti wa nani anaweza kufika darasani na tuna kamera za ufuatiliaji wa kinachoendelea.
Tunatoa chakula bora na vitafunwa, tukizingatia mahitaji ya lishe na mizio (aleji). Tuna ratiba zinazoweza badilishwa kama vile programu za siku nzima na zile za nusu siku. Ratiba hizi zinakidhi mahitaji ya wazazi ambao ni wafanyakazi. Lengo la Little Sprouts Moshi ni kusaidia ukuaji wa kiakili, kimwili, kijamii, na kihisia wa watoto.

HUDUMA YA KUTUNZA/KULEA WATOTO

Huduma yetu ya uangalizi wa watoto ni suluhisho kwa mahitaji ya wazazi wenye shughuli nyingi na wale ambao wapo safarini mjini Moshi. Walezi wetu wenye uaminifu na wataalamu hutoa huduma ya kiwango cha juu kwa watoto wa umri wote katika kituo chetu kilichopangiliwa vema kwa kazi hiyo hapa Moshi. Tukiwa na kipaumbele cha usalama na ushiriki wa watoto wote katika shughuli za kila siku kituoni, unaweza kuwa na hakika kwamba watoto wako watatunzwa vizuri wakati wewe unashughulikia majukumu yako. Tunakupa amani na kukurahisishia malezi, kiasi cha kufanya ulezi wa mtoto wako kuwa rahisi wakati unapokua upo hapa Moshi.

MATUKIO NA SHUGHULI MBALIMBALI KWA WATOTO

Little Sprouts Moshi inajitahidi zaidi kuandaa matukio na shughuli mbalimbali za kwa watoto. Tunaratibu sherehe za aina mbalimbali, shughuli za sanaa na ufundi, na ziara za kitalii ili kukuza ubunifu na mawazo ya watoto. Muda wa kucheza nje unakuza ukuaji wa kimwili na uwezo kushirikiana katika jamii. Matukio maalum wakati wa likizo yanajenga uzoefu wenye kumbukumbu, ambapo huwa tunasherehea siku kama Krismasi. Katika shughuli zote , usalama ni jambo la kipaumbele, na wafanyakazi wetu wamefundishwa vema kusimamia hilo.
Matukio na shughuli za Little Sprouts Moshi huwapa watoto nafasi ya kupata marafiki, kukuza stadi za kijamii, na kupata wakati wa kujifurahisha na kuburudika wakiwa chini ya uangalizi wetu.

JITOLEE KUFANYA KAZI NASI

Little Sprouts Moshi inakaribisha wakazi wa eneo hili na wageni kutoka nje kujitolea ili kuwa na mchango katika maisha ya watoto. Kama kituo cha utunzaji wa watoto, tunatoa fursa zenye thamani kwa watu binafsi wanaopenda kufanya kazi na watoto. Wanaotaka kujitolea wanapaswa kuwa na upendo wa dhati kwa watoto, uvumilivu, na kujisikia kulea watoto. Uzoefu katika utunzaji wa watoto au elimu ya utotoni unathaminiwa sana. Majukumu yanaweza kujumuisha kusaidia katika shughuli za kila za kituo chetu, kuwaongoza watoto katika michezo na kujifunza kwao, na kutoa msaada wa kitaalamu kwa wafanyakazi wetu. Little Sprouts Moshi inathamini dhamira na uaminifu wa wanaojitolea kufanya kazi katika kujenga mazingira salama na yenye kujenga ukuaji kwa watoto wanaokua chini ya uangalizi wao.

Little Sprouts

Kituo chako cha kutunza watoto cha kuaminika ndani ya Moshi na tumejikita kutoa huduma bora ya uangalizi watoto, tukiwapa mazingira salama, yenye kuvutia na kuelimisha. Walezi wetu wenye uzoefu, shughuli zenye kufurahisha watoto, na kujitoa kwetu kweli kweli kuhakikisha ukuaji wa watoto vinatufanya kuwa chaguo bora kwa wazazi wanaotafuta huduma bora kwa watoto wao.

Kampuni

Kuhusu sisi
wasiliana nasi
Mahali tulipo

Huduma

Day Care
Kuangalia watoto
Matukio na shughuli
Jitolee

Blog

Coming soon